Na Amiri kilagalila,Njombe
Serikali mkoa wa Njombe imezindua soko la uuzaji
wa madini ya dhahabu na vito kwa nia ya kudhibiti wimbi la utoroshaji wa madini
uliokuwa unafanywa na wachimbaji waliokuwa wakikwepa kulipa mapato ya serikali.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika
katika eneo la ofisi za madini mkoa wa Njombe zilizopo Nazareth kata ya mji
mwema halmashauri ya mji wa Njombe,mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole
Sendeka amesema kuwepo kwa soko hilo la madini itasaidia wachimbaji hao kutumia
fursa na njia zilizosahihi kulipa mapato kwa serikali.
“Kuanzisha soko la madini katika mkoa wetu
inakuwa ni fursa ya serikali katika kukusanya mapato yake yanayotokana na
madini, lakini pia eneo letu hili la soko la madini litakalokuwa pia eneo
linalotoa elimu ya uchimbaji wa madini kwa njia ya kisasa na kueleza
kuwaunganisha wananchi na wawekezaji wengine wenye nia ya kuwekeza mkoani
Njombe"alisema Ole Sendeka.
Ole Sendeka alisema mkoa wa Njombe unayo
rasilimali nyingi ya madini mbalimbali ikiwemo aina tofauti ya vito, hivyo ni
vyema wachimbaji wa madini wakaendelea kuhamasisha wawekezaji mbalimbali wakaja
mkoani hapa kuwekeza kwa maslahi mapana ya taifa.
“Nampongeza sana Rais Dkt. Magufuli kwa
kuhakikisha kwamba rasilimali na utajiri wa nchi yetu unatumika kwa
manufaa na maslahi mapana ya nchi yetu, sasa namna bora ya kumuunga mkono Rais
ni kuhakikisha madini yetu yanazalishwa bila kujali madini ya kiwandani madini
ya vito yanapitwa katika mfumo na yanauzwa katika utaratibu rasmi uliowekwa na
serikali”alisema Ole Sendeka.
Kwa upande wake,kamishina
wa madini mkoa wa Njombe, Wilfred Machumu alisema mkoa wa Njombe changamoto
iliyopo kwa sasa ni utoroshaji wa madini kwenye baadhi ya maeneo yaliyopo
mkoani humo hali inayosababisha kuikosesha mapato serikali.
“Utoroshaji wa madini upo mkubwa sana katika mkoa
wa Njombe,hasa maeneo ya Uwemba,Lola Lupembe na Mfumbi Makete, yale maeneo
ndiyo yanayotusumbua sana na hayo ndiyo takwimu zinaonyesha kuwa ndiko kwenye
utoroshaji mkubwa sana,tumepanga kuongeza nguvu katika kuyafatilia maeneo hayo
kuhakikisha hakuna jambo hilo"alisema Machumu.
Baadhi ya wachimbaji wa madini akiwemo Abusalum
Sanga walimweleza Ole Sendeka kuwa mkoani Njombe rasilimali ya madini ni nyingi
isipokuwa changamoto iliyopo ni kukosekana kwa vifaa vya kusaidia uchimbaji wa
madini ya aina mbalimbali kwenye mkoa wa Njombe ikiwemo madini aina ya shaba
ambayo walisema iko kwenye ubora wa juu tofauti na maeneo mengine hapa nchini.
“Tatizo linalotukwami sisi wachimbaji hapa Njombe
ni kukosekana kwa mashine ambazo zingekuwa mkombozi mkubwa na tungekuwa mbali
sana kwenye uchimbaji wa madini hapa mkoani, dhahabu iliyopo kata ya Ibumi ni
nzuri na safi lakini kikwazo ni vifaa vya kuchimbia vinatuangusha"alisema
Sanga.
Kwa upande wa mwenyekiti chama cha wachimbaji
madini mkoa wa Njombe Alfred Luvanda alisema soko hilo litajenga imani ya
uwekezaji sekta ya madini kwa wakazi wa mkoa huo kinyume na hapo awali
0 Comments