TANGAZA NASI

header ads

Naibu waziri wa mambo ya ndani Hamadi Masauni ajitosa kuchukua fomu ya Urais Zanzibar



Zanzibar.

NAIBU Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Unguja, Hamadi Yusuf Masauni amajitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM.

Mhandisi Masauni anakuwa mgombea wa 19 kufika katika ofisi kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Mjini Unguja kwa ajili ya kuchukua fomu hizo za kugombea nafasi ya Urais.

Mara baada ya zoezi la uchukuaji wa fomu Mhandisi Hamadi Yusuf Masauni alisema kwamba  ameamua kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu na kuistawisha Zanzibar.

“Leo tarehe 22 Mimi hamadi masauni nmekuja kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais, huku nikitambua  nafasi hii ni kubwa ,ngumu na  lakini dhima yangu kuleta na kustawisha maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii” alisema Masauni.

alisema kwamba Pindipo atapata ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Urais na kuchaguliwa na waanchi atakidhi matakwa ya wananchi wa Zanzibar na Wajamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Post a Comment

0 Comments