Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe,Mwita Waitara amefafanua taarifa za kuumwa kwake kutokana na taarifa zinazosambaa mitandaoni zikieleza yeye kuumwa homa kali ya mapafu inayotokana na virusi vya Corona.
Waitara kupitia Kituo cha radio cha East Afrika amenukuliwa akisema
"Kuumwa ninaumwa,nimelazwa hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma,lakini kwamba naumwa nini mimi sijui kwasababu bado sijapata taarifa ya wataalamu"Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe,Mwita Waitara akifafanua taarifa za kuumwa
#NjombePressUpdates
"Mimi taarifa za Corona sina,huyo aliyeandika unaweza ukamhoji,hali yangu haikuwa nzuri sana na kabla ya hapo nilikuwa siwezi kuongea na simu"Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe,Mwita Waitara akifafanua taarifa za kuumwa
#NjombePressUpdates
"Naumwa tu kawaida kwasababu tangu nimekuwa Naibu waziri nimezunguka sana,sijawahi kupewa likizo wala kupumzika kwa hiyo niliona ni uchovu tu wa mwili na mwili kuishiwa nguvu"Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe,Mwita Waitara akifafanua taarifa za kuumwa
#NjombePressUpdates
"Kama kuna mtu anataka taarifa. Hospitali nimelazwa ya Serikali,wapimaji wapo, na mimi mwenyewe nipo"Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe,Mwita Waitara akifafanua taarifa za kuumwa.
#NjombePressUpdates
0 Comments