Mkuu
wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka wakati akitoa wiki mbili kurejeshwa
ardhi ya wazee iliyotaka kupokwa.
Mkuu
wa mkoa wa Njombe akiwa katika maeneo ya wazee yaliyodaiwa kuuzwa bila kufuata
utaratibu na kuirejesha kwa mzee huyo.
Bi.
Doris Kaluwa wakati akitoa taarifa juu ya ardhi yake iliyodaiwa kuuzwa na mmoja
wa ndugu yake bila kufuata utaratibu.
Christopher
Mwigune mmoja wa wanunuzi wa ardhi hiyo akizungumza taratibu alizotumia kupata
ardhi.
Mkuu
wa idara ya ardhi wa halmashauri ya mji
Njombe, Lusubila Mwakafuje akitoa ufafanuzi namna ya upataji wa ardhi.
Na
Amiri kilagalila,Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ametoa wiki mbili kwa watu wanne
kurejesha ekari mbili za ardhi ya wazee wawili wanaokadiliwa kuwa na miaka
zaidi ya 80 zilizouzwa kimakosa, ambayo
walipewa zawadi na serikali ya mtaa wa Mji mwema kutokana na kuamsha ari ya
taaluma.
Eneo hilo lenye ukubwa ekari 2 linadaiwa kuuzwa na mtu wa jirani wa wazee hao miaka minne iliyopita anaefahamika kwa jina George Angeli ,hatua ambayo imesababisha kuidai haki yao katika vyombo vya sheria.

Ole Sendeka ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea kilio cha wazee hao na kuamua kutembelea eneo lenye mzozo na kudhibitisha uhalali wa umiriki wao ambapo amesema endapo walionunua eneo hilo watahitaji fidia wamfate aliewauzia.
“Msitafute mgogoro na mimi,ninatoa wiki mbili kila mmoja aondoe kilichopo hapa,unataka fidia yako mfuate aliyekuuzia ardhi”alisema Ole Sendeka
Aliongeza
kuwa
“Kwa
ushahidi wa maandishi na kwa maelezo ya walio kuwepo,ardhi hii ilitolewa kwa
mr. na mr’s Kalua baada ya wao kustaafu kwenye utumishi kwa nafasi ya ualimu”alisema
Ole Sendeka
Mzee Doris Kaluwa na Joseph Kaluwa ambao ni wanafamilia na walimu wastaafu wanasema eneo walilopokwa walipewa na serikali mtaa wa Mjimwema kutokana na mchango wao katika elimu na kudai kwamba uamuzi wa kuliuza eneo hilo haujabarikiwa na wao.
“Sisi hatukumtuma mtu atuuzie viwanja kama tungemtuma tungekuwa tumeenda kwenye ofisi ya kijiji ili waliuziana tu barabarani na sisi tulipata hii ardhi kama zawadi hapa mji mwema”alisema Doris Kaluwa

Wakati wazee hawa wakidai haki yao na serikali kutoa maagizo , Christopher Mwigune ambaye ni moja kati ya watu waliouziwa eneo hilo kimakosa wanasema busara inahitajika kutatua mzozo huo huku mkuu wa idara ya ardhi halmashauri ya mji wa Njombe Lusubila Mwakafuje akidai utaratubu ulivunjwa katika mauziano ya ardhi hiyo.
“Sisi tulikuaja tukanunua kwa mtu lakini inawezekana kweli hiyo changamoto imejitokeza na tayari tumeshawekeza,mimi ombi langu ni hekima inaweza ikatumika”alisema Christopher Mwigune
Kwa
upande wake mkuu wa idara ya ardhi wa halmashauri
ya mji Njombe, Lusubila Mwakafuje amesema wanunuzi walionunua viwanja kwenye
ardhi ya walimu hao wastaafu hawakufuata utaratibu mzuri.
“Eneo
lolte linapotaka kuuzwa au watu wowote wanaotaka kufanya mauziano ni vema
wakapata muongozo kutoka serikali ya mtaa”alisema Lusubila Mwakafuje
0 Comments