Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson, amesema kuwa mmoja wa Wabunge wa Bunge hilo amethibitika kuwa ana maambukizi ya Virusi vya Corona.
Taarifa
hiyo ameitoa mchana wa leo wa Aprili 20, 2020, wakati akiahirisha
Mkutano wa Tisa kikao cha 12 cha Bunge hilo Jijini Dodoma, na kuwataka
Wabunge kuzingatia kanuni zote za afya zilizotolewa ikiwemo kila Mbunge
kukaa kwenye kiti chake na siyo sehemu ya mtu mwingine.
"Tumepata
taarifa kuwa mmoja wetu tayari amepata maambukizi ya COVID-19, mgonjwa
huyo anaendelea vizuri na Serikali inaendelea kumuangalia na kumpatia
matibabu stahiki, na maelezo ya Mbunge huyo alisafiri kwenda Dar es
Salaam siku za hivi karibuni" ameeleza Naibu Spika.
Kwa
mujibu wa Dkt Tulia ameeleza kuwa Mbunge huyo alianza kujisikia vibaya
kuanzia Jumatano ya wiki iliyopita kwa kuona dalili zote za ugonjwa huo
na hatimaye alipofanyiwa vipimo alibainika kuwa na ugonjwa huo.
"Kwa maelezo ya Mbunge huyo ni kwamba alisafiri kwenda Dar es Salaam na aliporejea kuanzia Jumatano alianza kuhisi dalili kama zilivyotangazwa na baada ya kupimwa ilithibitishwa kuwa amepata maambukizi ya virusi vya Corona" Naibu Spika-Tulia Ackson

0 Comments