Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe (NPC), Nickson Mahundi amewataka wanahabari mkoani Njombe pamoja na wilaya zote kufanya kazi zao kwa kuchukua tahadhari kubwa na kuepuka mikusanyiko wakati wa kutafuta habari ili kuepukana na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19)
Mahundi amesema wanahabari mkoani hapo wanatakiwa kuchukua tahadhari kubwa za kulinda maisha yao ikiwemo kuzingatia masharti ya wataalam wa wizara ya afya ya kujikinga na maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Covid 19 ili waweze kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu kujikinga na Corona.
Hamis Kassapa ni katibu mtendaji wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe anasema waandishi wa habari wanapotekeleza majukumu yao ya kihabari ni vyema wakachukua tahadhari sio tu kwa kuepuka kupata maambukizi kwenye vitendea kazi vyao bali hata familia zao.
Baadhi ya wanachana wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe,akiwemo Elizabeth Kilindi anasema wanahabari waache mzaha na wazingatie taarifa za wataalam wa afya kwa kuwa bado wana jukumu kubwa la kutoa elimu kwa jamii juu ya virusi vya Covid-19
0 Comments