Mtangazaji wa muda wa shirika la CNN, Richard Quest, amefichua kwamba anaugua virusi vya Corona.
Mhariri huyo wa biashara, ambaye huendesha kipindi cha Quest Means Business, alianika habari hizo kuwa amepatwa na ugonjwa huo siku ya Jumatatu, Aprili 20.
Kupitia mitandao ya kijamii, Quest alitangaza kuwa alipatwa na COVID-19 na hakuwa na dalili kubwa ya ugonjwa huo.
Katika ujumbe kwenye Twitter, mwanahabari huyo alisema anawaombea watu wasiojiweza na kuwashauri mashabiki wake kuwa salama.
"Nimeshikwa na coronavirus. Ninafurahi kuwa nina dalili chache, kukohoa tu. Ninawaombea wasiojiweza. Kaa ndani na okoa maisha," aliandika Quest.
Vile vile katika video fupi kwenye Instagram, mwanahabari huyo wa New York alisema alianza kukohoa wikendi na kuamua kufanyiwa vipimo.
Kulingana na Quest, hakukumbana na matatizo ya kupumua ama joto jingi mwilini huku akisema daktari wake alimwambia kuwa atapona kabisa.
"Sijakuwa na matatizo ya kupumua, joto jingi mwilini ama kutokwa na jasho.Kweli nina bahati. Daktari wangu alisema nitapona kikamilifu. Niko njiani," alisema Quest.
Chanzo.Tuko kiswahili
0 Comments