TANGAZA NASI

header ads

Madaktari wa kijeshi waondoka Wuhan,baada ya kumaliza kuwahudumia wagonjwa wa Covid-19



Kufuatia idhini iliyotolewa na Rais Xi Jinping wa China, vikosi vya madaktari wa kijeshi wameanza kuondoka Wuhan baada ya kumaliza jukumu la kuwatibu wagonjwa wa virusi vya Corona mjini humo.

Tarehe 24, Januari, Rais Xi Jinping ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Kijeshi ya CPC, alitoa agizo muhimu la kuyataka majeshi na vitengo tofauti vya kijeshi kupeleka madaktari na wahudumu wa afya mjini Wuhan, mji ulioathiriwa zaidi na maambukizi ya virusi vya Corona nchini China.

Madaktari wanajeshi wapatao elfu nne walipelekwa kwa awamu tatu katika hospitali tatu mjini Wuhan, na kupokea magonjwa 7,198 wa virusi vya Corona, na hakuna daktari aliyeambukizwa virusi.

Wakati huohuo, wataalam wa matibabu wa kijeshi pia wamejitahidi kufanya utafiti wa kisayansi na kufanikiwa kubuni chanjo ambayo tayari imeingia kwenye kipindi cha majaribio ya kliniki.


Post a Comment

1 Comments