Na Amiri kilagalila,Njombe
Kaido Mfilinge anayekadiliwa kuwa na umri wa mika 30, ambaye inadaiwa ni mganga wa kienyeji kwa asili amekutwa amejinyonga mpaka kufa katika mtaa wa Nazaleti mjini Njombe baada ya kuchukua dawa kwa mganga mwenzie kutoka mkoani Ruvuma na kukiuka masharti ambayo alikuwa amepewa.
Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema jeshi la polisi limefika katika eneo ambalo kijana huyo amejinyongea na kumkuta ameacha barua ambayo inasema nimejinyonga baada ya kusumbuliwa na kibuyu ambacho nilikuwa nimepewa na mganga na kusababisha mizimu kuanza kusumbua.
“Huyu kijana yeye ni mganga wa kienyeji kwa asili yake na amejinyonga baada ya kwenda mkoa wa Ruvuma akapewa dawa iliyokuwa na masharti,ile dawa aliyoenda nayo nyumbani kwake kibuyu kimoja kikaanza kumsumbua akamuuliza Yule aliyempa akaambiwa akatupe kwenye njia panda yoyote”alisema kamanda Hamis Issa
Kmanda Issa ameongeza kuwa
“Lakini yule kijana akaamua kuchukua maamuzi magumu akajinyonga na haya maneneo ninayoyaongea ameyaandika mwenyewe kwenye karatasi yake samahani mizimu nimekosea masharti,samahani familia yangu,samahani mganga wangu uliyenipa masharti nimekosea nimeaamua kujitoa duniani kwa kujinyonga na hiyo karatasi ipo imeandikwa hivyo”alisema Kamanda Issa
Aidha kamanda Issa amesema kuwa jeshi hilo pia limekata vitu vya wizi vilivyoibwa katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Ruvuma,Mbeya,Iringa na Njombe zikiwemo TV zaidi ya 16,Jenereta,vyombo vya muziki.
“Kuna vitu mbali mbali kuanzia TV zilizoibwa hapa Njombe na zingine kwa watu maarufu kwa hiyo tunaomba watu waje kuzitambua”alisema Hamis Issa
Katika tukio lingine kamanda huyo amesema kikosi cha jeshi la polisi kinachofanya kazi kwa karibu na wananchi kutoka maeneo mbalimbali kimekamata watu watatu katika mtandao hatari wa wezi ambao umekuwa ukifanya matukio ya wizi hadi kwa viongozi wa serikali pamoja na makanisa.
“Mtandao huu unamshirikisha mtu mmoja anaitwa Dickson Mshele huyu ana kikundi cha vijana ambao ni wezi wakivunja majumba ya watu wanamkusanyia yeye ana gari aina ya Dimsam inabeba usiku kwa usiku inapeleka Songea na kule kuna mtu mmoja anaitwa Hasan yeye ni fundi Tv zikifika kule anazibadilisha sula”alisema Kamanda
0 Comments