TANGAZA NASI

header ads

Kauli ya Mwakalebela baada ya kufungiwa miaka mitano kujihusisha na soka

 


BAADA ya jana Aprili 2, Kamati ya Maadili ya Shirikisho la  Mpira wa Miguu, Tanzania, (TFF) kummfungia miaka mitano Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kujishughulisha na masuala ya mpira wa miguu ndani na nje ya nchi, kiongozi huyo amesema kuwa alijua ingekuwa hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na TFF Aprili 2 imeeleza kuwa kamati imemkuta na hatia ya kutoa maneno ya uchochezi kwa Wanachama na mashabiki kuhusu vyombo vinavyosimamia mpira.

Mwakalebela amesema kuwa ameambiwa kwamba asijihusishe na masuala yoyote yanayohusu michezo.

"Nimeambiwa nisijihusishe na masuala yoyote yale yanayohusu michezo, yaani iwe kwenye magazeti ya michezo nimeambiwa nisisome hata magazeti ya michezo.

"Ikiwa ninatazama TV ikifika wakati wa michezo nisiangalie, niliwaambia viongozi wangu kwa namna mwenendo ulivyokuwa basi ningefungiwa kwa namna mambo ambavyo yalikuwa yanakwenda.

"Nimekuwa nikiitetea Yanga katika masuala ya michezo na kila ambacho nimekuwa nikifanya ni kwa sababu ya Klabu ya Yanga,".

Post a Comment

0 Comments