TANGAZA NASI

header ads

Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 03.04.2021

 


Liverpool inakabiliwa na hali ya sintafahamu kumhusu mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, huku baadhiya wadau katika klabu hiyo wakizidi kushawishika kwamba nyota huyo aliye na umri wa miaka 28-anatazamia hatma yake ya siku zijazo mahali pengine. (ESPN)

Manchester United na Chelsea zinamsaka winga wa Real Madrid Mhispania Lucas Vazquez, 29. (ABC)

Chelsea wanataka kumnunua mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 32, atakapoondoka Manchester City msimu huu wa joto ikiwa tamkosa mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 20, kutoka Borussia Dortmund. (ESPN)

Real Madrid wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Martin Odegaard, 22, ili kufadhili uhamisho wa Haaland. Odegaard kwa sasa anachezea Arsenal kwa mkopo na Gunners wanataka kumpatia mkataba wa kudumu. (Times)

Lakini Haaland ameripotiwa kuiambia Real Madrid kwamba anataka kuwa kikosi kimoja na Odegaard msimu ujao. (Star)

Barcelona huenda wakamnunua mshambuliaji wa Inter na Argentina Lautaro Martinez, 23, ikiwa juhudi zao za kumsaka Haaland hazitafua dafu. (Sport)

Paris St-Germain huenda wakamwachilia mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, msimu huu wa joto endapo mazungumzo kuhusu mkataba wake yataendelea kukwama. (Le Parisien)

Barcelona wanapania kusitisha kampeni yao ya kumsaka kiungo wa kati wa Liverpool Mholanzi Georginio Wijnaldum, 30, na badala yake kumpatia nafasi muhimu kinda wa Uhispania Ilaix Moriba,18, msimu ujao. (Metro)

Juventus wanataka kumrudisja mshambuliaji wa Everton na Italia Moise Kean, ambaye sasa yuko kwa mkopo Paris St-Germain. Kiungo huyo aliye na umri wa miaka 21-alijiunga na Toffees kutoka Juve mwaka 2019. (Tuttosport - in Italian)

Post a Comment

0 Comments