Moja kati ya taarifa inayo-trend kwa sasa mitandaoni ni kuhusu msanii wa filamu Kajala Masanja na msanii wa muziki Harmonize ambao inasemekana penzi lao limefika mwisho kutokana na baadhi ya viashiria vya mazingira vilivyojitokeza.
Taarifa hiyo imekuja baada ya Kajala Masanja kufuta picha zote alizowahi ku-post akiwa na Harmonize kwenye mtandao wa Instagram kisha kumu-unfollow kwenye mtandao na kuandika ujumbe wa Kiingereza uliotafsirika kama
"Usimuumize mtu kwa ajili ya sababu zako binafsi"
Mahusiano ya Harmonize na Kajala yalikuja kwa kasi na yalivutia watu wengi hadi kufikia hatua ya kuchorana tattoo japo baadhi ya watu wengine walikuwa wanalipinga penzi lao mitandaoni.
0 Comments