Na Salvatory Ntandu - Ushetu
Katika
jitihada za kupambana na Ugonjwa wa homa kali ya Mapafu
inayosababishwa na virusi vya Corona, Kanisa la Kiinjili la kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini Mashariki ya ziwa Victoria limetoa
Msaada wa vifaa vya kujikinga dhidi ya COVID 19 kwa waganga wa tiba
asili vyenye thamani ya shilingi Milioni 3.5.
Akizungumza
katika hafla maalum ya kukabidhi vifaa hivyo Jana na Askofu wa
Dayosisi hiyo Dkt, Emmanuel Joseph Makala kwa Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Ushetu Michael Matomora alisema kuwa, Kanisa limetoa vifaa hivyo kwa
waganga hao ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa huo katika
maeneo yao ya kazi.
Alisema
,Kanisa limebaini kuwa waganga wa tiba asili, wanafanya kazi katika
mazingira hatarishi kutokana na kuhudumia wateja wao bila ya kuwa na
vifaa maalumu vya kujikinga na ugonjwa wa COVID 19 kama vile vitakasa
mikono, ndoo za maji na barakoa.
“Kundi
hili ni Muhimu hivyo,kanisa limeamua kuwajali kwa kutoa vifaa hivi
katika mikoa mbalimbali ya kanda ya ziwa kwa kuanza na Bariadi mkoa wa
Simiyu na Ushetu mkoa wa Shinyanga ili ,kuunga mkono juhudi za serikali
katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu”,alisema Dkt Makala.
Awali
akipokea vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Michael
Matomora alilishukuru kanisa la KKKT kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo
vitatumika na waganga wa jadi na vingine vitapelekwa katika kituo cha
afya Ukume ili kuwa kinga wagonjwa wanaokwenda kupata huduma katika
maeneo hayo.
Alifafanua
kuwa Ofisi yake itahakikisha vifaa hivyo vinawafikia waganga wote wa
tiba asili sambamba na kuyaomba mashirika mengine kuiga mfano wa kanisa
la KKKT kwa kuendelea kutoa vifaa vya kujikinga na COVID 19.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa waganga wa Tiba Asili katika Halmashauri
hiyo, Shumileta Charles alisema wanaendelea kuzingatia maelekezo ya
serikali katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na
wanahakikisha kabla ya kutoa huduma wateja wao wananawa mikono na kuvaa
barakoa.
“vifaa
hivi vilivyotolewa na kanisa vitasaidia kuwakinga waganga wa tiba
asili dhidi ya janga la Corona na nichukue fursa hii kupitia vyombo vya
habari kuwataka wazingatie maelekezo ya serikali ili kujikinga wao na
pindi wanapokuwa wanawahudumia wateja wao,”alisema Charles.
0 Comments