Mtangazaji kipindi cha XXL cha Clouds FM, Kenedy The Remedy amepata ajali ya gari na sasa hali yake inaendelea vizuri.
Katika ujumbe ambao amechapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji.
Ujumbe wa Kenedy
"Mungu ni mwema mno, na siwezi kumshukuru vya kutosha kwa upendo wake na rehema juu yangu, familia yangu na wanaonizunguka, licha ya udhaifu wangu wote kanipa nafasi nyingine ya kuishi ;.
Nawashukuru Sana wasamaria wema na Polisi walionipa msaada baada ya kupata ajali, wakanitunzia kila kitu mpaka familia yangu ilipofika.
Shukrani kwa madaktari wote kunitibu na walionifanyia upasuaji Dr. Sam, Dr. Sadot kutoka Rabinisia Memorial Hospital Tegeta na wauguzi wote walionisaidia. Shukrani za kipekee ziende kwa walionitoa uoga nikubali upasuaji Mama la mama Sylvia a.k.a mshika pesa zangu , My brother Yahya a.k.a Nguli, Dr. Issac Maro toka TMH, Dr. Sizya toka Muhimbili Hospital.
Ndugu, Jamaa na Wafanyakazi wenzangu walioniombea kwa namna yoyote ile nirejee kwenye hali yangu ya kawaida pia nawashukuru  Naendelea poa ngoja nivute pumzi kidogo ntarejea kuliamsha ka kawa kwenye Familia Kubwa Kuliko XXL
Hata hivyo bado taarifa zinaeleza moja ya watangazaji wa kipindi cha asubuhi power breakfast Bonge,naye anaendelea vizuri kutokana na ajali aliyoipata hivi karibuni.
Credit:bongoswagz.com
0 Comments