TANGAZA NASI

header ads

Diamond kuchangia kodi ya pango kwa kaya 500 nchini


Msanii Nyota wa muziki wa kizazi kipya a.k.a BongoFleva Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz, amesema kuwa atachangia ‘kodi ya pango’ kwa kaya 500 nchini kwa ajili ya kupunguza makali ya kiuchumi wakati huu ambapo Watanzania wanapambana dhidi ya virusi vya Corona (Covid-19).

''Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususani upande wa biashara, nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo magumu kwa wengi wetu... na mimi ni miongoni mwa walio ndani ya janga hili,'' ameeleza Diamond kwenye ukurasa wake Instargram

Kupitia ukurasa wake wa  Instagram,Msanii huyo ambaye amejizolea sifa lukuki ndani na je ya nchi ,Diamond amebainisha kuwa katika kulifanikia zoezi hilo utaratibu zaidi utatangazwa siku ya Jumatatu ya namna kaya hizo 500 zitakavyopatikana na kuweza kupata msaada huo.

Diamond Platnumz anakuwa msanii wa kwanza nchini kujitokeza hadharani na kuweka bayana kuwa atasaidia chochote wakati huu wa janga la mlipuko wa virusi vya corona vyenye kusababisha homa kali ya mapafu yaani #COVID-19.

Post a Comment

0 Comments