Majimbo
matatu nchini Marekani yameruhusu baadhi ya maduka kufunguliwa tena baada ya
hatua zilizowekwa za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona, huku idadi
ya vifo nchini humo ikizidi watu 51,000.
Saluni za wanaume na wanawake
sasa zinaweza kufunguliwa tena katika majimbo ya Georgia Oklahoma huku Alaska
ikiondoa masharti iliyokuwa imewekea migahawa.
Ijumaa rais Donald Trump
aliondoka mapema kuliko ilivyo kawaida wakati otuba yake ya kawaida kuhusu
maendeleo ya hali ya janga la corona, akakataa kupokea maswali ya waandishi wa
habari.
Rais Trump amekabiliwa na
ukosoaji mkubwa baada ya kupendeza kuwachoma sindano ya kemikali za kuua
vimelea au za usafi wagonjwa wa corona inaweza kuwa ni jambo la manufaa.
Kauli zake zimekua zikilaaniwa na
madaktari pamoja na watengenezaji wa bidhaa wanaozitaja kuwa ni za hatari.
Kemikali za kuua vijidudu au vimelea zinaua na zinaweza kuwa sumu zikiingizwa
katika mwili wa binadamu , na hata matumizi yake ya nje ya mwili yanaweza kuwa
hatari kwa ngozi, macho na mfumo wa kupumua.
Bwana Trump alisema siku ya
Ijumaa kuwa kauli-alizozitoa katika mkutano wa wanahabari siku moja kabla
zilikuwa za vichekesho na muktadha wake ulipotoshwa.
Wateja wanaotembelea biashara
mpya zilizofunguliwa katika majimbo ya Georgia, Oklahoma na Alaska watatarajiwa
kuendelea kuheshimu hatua za kutosogeleana .
Lakini baadhi ya miji na maeneo
wameamua kuendelea kutekeleza hatua yao ya kukaa nyumbani.
Katika jimbo la Georgia, ambalo
lina moja ya ratiba ya haraka sana ya kufungua shughuli nchini humo ,saluni za
wanaume na wanawake, za kutengeneza kucha , tatuu, na biashara nyingine za
mapodozi zitaruhusiwa kufungua shughuli zake.
Siku ya Jumatatu migahawa ya
chakula na kumbi za michezo zitaruhusiwa kufunguliwa tena.
Huku kukiwa na madai ya ukosefu
wa ajira kwa watu milioni 26-au takribani 15% ya watu wa Marekani - tangu
katikati mwa mwezi Machi, majimbo menfufua biashara zilizositishwa kutokana na
janga la corona.
Lakini wataalamu wa afya wameonya
kuwa hatua hizo huenda zikawa zimechukuliwa mapema, huku kukiwa na hofu kwamba
zinaweza kusababisha wimbi jingine la maambukizi.
Baada ya kukosolewa na
Trump,Gavana wa jimbo la Georgia Brian Kemp amri kali za usafi na watu
kutosogeleana kuhusu kuhusu migahawa.
Katika hotuba ya White House
iliyodumu kwa muda wa dakika 20,Bwana Trump aliwaomba watu kuendelea kufuata sheria
zinazohusu kutotengamana kwa watu katika jamiina kutumia barakoa.
Pia Ijumaa, Bwana Trump pia
alisaini muswada wa thamani ya bilioni 484 (Pauni Bilioni 391) za kuchochea
uchumi , akisema kuwa anataka "kuharakisha nafuu ya kiuchumi kwa ajili ya
raia wetu".
Ni msaada wan ne wa Covid-19
ikupima virusi, hospitali na mpango wa mikopo ya biashara ndogondogo.
Marekani ina idadi kubwa zaidi ya
vifo na visa corona kuliko nchi nyingine duniani- zaidi ya vifo 50,000 na visa
890,000 vimethibitishwa.
Lakini nchi za Ulaya, mkiwemo
Uhispania na Italia, zimerekodi vya juu zaidi ikilinganishwa na idadi ya watu
kuliko Marekani ambayo ina jumla ya watu milioni 330.
Kupanda haraka kwa hivi karibuni
kwa idadi ya vifo kwa sehemu kubwa ni kujumuishwa kwa "labda" kwa
idadi ya vifo - Tarehe 14 Aprili, Kituo cha Marekani udhibiti wa magonjwa
kilisema hesabu ya visa vya maambukizi itajumuisha visa vilivyothibitishwa na
visa vinavyoshukiwa pamoja na vifo kwa pamoja.
Kifo kinachoshukiwa kuwa
kimetokana na Covid-19 ni mojawapo ya vile vinavyodhaniwa kimatibabu lakini
bado havijathibitshwa.
Pia ni muhimu kutambua kuwa visa
vingi ambavyo muathiriwa hupati madhara vinasalia kutotangazwa, kwa hiyo
kiwango visa vya vifovilivyothibitishwa sio sawa na kiwango cha vifo
vinavyosababishwa na ugonjwa wa corona kwa ujumla.
Juhudi za kupima ni muhimu katika
kutafuta visa halisi vya vifo na jinsi ugonjwa unavyosambaa. Makamu rais Mike
Pence, ambaye ni kiongozi wa kikosi kazi cha kupambana na Covid-19, alisema
kuwa Marekani imewapima watu 4.9 hadi sasa, na kwamba serikali inashirikiana na
magavana kupanua zaidi upimaji wa virusi wa virusi vya corona.
Chanzo:BBC
0 Comments