TANGAZA NASI

header ads

Historia fupi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa
mnamo tarehe 26 Aprili, 1964 kwa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja).

Tanganyika ilikuwa ni
mwendelezo wakoloni la Ujerumani, utawala wa Waingereza kwa Mamlaka ya Umoja wa Mataifa, Himaya ya Umoja wa Mataifa chini ya utawala wa
Uingereza na mwisho Taifa huru kuanzia mwaka 1961 ndani ya nchi za Jumuiya ya Madola.

Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar ziliingia mkataba wa Muungano mnamo
mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.

Mkataba huu wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu
Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar.

Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika
na Baraza la Mapinduzi hapo tarehe 26 Aprili, 1964
na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee
Jijini Dar es Salaam na kubadilishana Hati za
Muungano.

Sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 4 kwamba: “Jamhuri ya
Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za
Muungano).

Jina hili la 'Jamhuri ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar' lilibadilishwa baadae mnamo tarehe 28 Oktoba, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka
1964.

Makala hii kwa msaada wa mitandao.

Post a Comment

0 Comments