TANGAZA NASI

header ads

COVID-19:Samatta na wenzake kukatwa 25% ya mshahara


Wachezaji wa Aston Villa nchini Uingereza wamekubali kukatwa mshahara kwa asilimia 25 kwa kipindi cha miezi minne kwa ajili ya kuinusuru klabu yao kiuchumi wakati huu janga la Virusi vya Corona.

Hata hivyo klabu hiyo itaendelea kuwalipa watumishi wengine wa chini mishahara yao kama ilivyo kwa kipindi chote ambacho watu hawaruhusiwi kutoka nje (Lockdown).

Kwa sasa kutokana na Virusi vya Corona Ligi mbalimbali duniani zimesimama, huku Ligi ya Uingereza ikielezwa kuwa kuna uwezekano wa kurejea Juni 8 mwaka huu.

@BongoSwaggz

Post a Comment

0 Comments