Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilayani ya Njombe Ally Juma amewahakikishia wananchi na wapiga kura katika jimbo hilo kuwa maandalizi yote ya kuelekea uchaguzi mkuu yamekamilika na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo ili kuwachagua viongozi watakao wahudumia kwa miaka mitano.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema hii leo Ally Juma amesema kuwa jimbo la Lupembe lenye vituo 154 limeakamilisha maandalizi yote ikiwemo kuweka mazingila mazuri kwa watu wenye mahitaji maalumu mara tu wafikapo katika vituo vya kupigia kura.
"Vifaa vyote vinavyohitajika vimefika na tayari sisi tumeviondoa kwa ajili ya kwenda kwenye maeneo husika,tunashukuru sana serikali na tume kuhakikisha zoezi hili linakamilika vizuri"alisema Ally Juma
Aidha mkurugenzi huyo amesema kuwa katika kuhamasisha Wananchi kujitokeza kupiga kura wamefanyajitihada maalumu ili kuhakikisha taarifa rasmi zinazohusu uchaguzi Zinawafikia wananchi ikiwemo kutumia makanisa,misikii,pamoja na kutumia ngoma za asili.
"Tulikuwa na mafunzo ya wasimamizi na yamekamilika na wamepata ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kufanya kazi hapo kesho kwa waledi wa hali ya juu na ni imani yetu katika jimbo la Lupembe uchaguzi utakuwa wa huru na haki.tumefanya hamasa za kutosha kwenye maeneo yetu kwa kutumia njia mbali mbali ili kuhakikisha wanachi wetu wanapata taarifa na habari za kutosha"aliongeza Ally Juma
Baadhi ya wananchi mkoani wamesema
"Mimi nimejiandaa vizuri kwa ajili ya kutumia haki yangu ya kidemokrasia na kupiga kura na kadi yangu nimeshaiandaa ili nikachague kiongozi atakayeniongoza kwa miaka mitano"alisema Dora Kacheche Mkazi wa Njombe
Jimbo la Lupembe lina takribani vituo 154 ambavyo vinataraji kupokea wapiga kura hapo tarehe 28 Octomber mwaka huu.

0 Comments