Mtaalam
wa halmashauri ya mji wa Njombe akiendelea na zoezi la kunyunyiza dawa kwenye
mabasi stendi ya Njombe mjini.
Na
Amiri kilagalila,Njombe
Mkuu
wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameagiza kila mwananchi kuhakikisha anapambana
na virusi vya Corona (COVID-19) kwa
hiari ili taifa liweze kubaki salama.
Msafiri
ametoa agizo hilo mapema alfajiri ya leo April 22 2020 wakati akiongoza zoezi
la utakasaji mabasi yanayoelekea mikoa mingine kutokea kituo cha mabasi Njombe
mjini kwa Croline,zoezi ambalo limeratibiwa na halmashauri ya mji wa Njombe.
“Kila
mwananchi ajione ni mdau katika zoezi la kupambana na virusi hawa na
kuhakikisha hawafiki kwetu,na kila mmoja awe tayari kushiriki zoezi hili kwa
hali na kwa hiari kama tulivyopambana vita vya Kagera ili taifa letu libaki
salama”alisema Ruth Msafiri
Aidha
ametoa wito kwa halmashauri ya mji wa Njombe kuweka utaratibu endelevu wa
upuliziaji dawa magari katika stendi hiyo huku akipongeza uongozi wa
halmashauri hiyo kwa kujitoa na kutafuta vitakasa magari kwa ghalama naafuu.
“Nichukue
nafasi kwa kuipongeza halmashauri ya mji wa Njombe kwa kujiongeza yenyewe na
kuona inaweza ikajaribu kufanya zoeze hili,tutaliwekea utaratibu mzuri liwe
endelevu na ninampongeza mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe pamoja na
wafamasia wake walivyobuni ule utaraibu wa kitaalam wakitupatia vitakasa magari ambavyo vina ghalama naafuu”alisema
tena Ruth Msafiri
Mganga
mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe Dkt,Isaya Mwasubila amesema
swala hilo la upuliziaji dawa ni nyongeza katika mapambano dhidi ya
virusi vya Corona na litaendelea sambamba na njia nyingine ili kuhakikisha mji
wa Njombe unakuwa salama.
“Zoezi
tulilofanya lina tija kubwa lakini sawala hili la upulizaji litakwenda pamoja
na mikakati yote kuleta tija kwa asilimia mia moja kwa hiyo si swala la kunawa
mikono peke yake ila ni kwa ujumla wake ili wananchi wetu wajue namna ya
kujikinga na kuhakikisha mji wetu wa Njombe unakuwa salama”alisema Mwasubila
Petro
Ndendya ni mmoja wa madereva wa mabasi ya safari ndefu ambaye basi lake
limeweza kunyunyiziwa dawa,amepongeza halmashauri ya mji wa Njombe kwa hatua
hiyo kwa kuwa magari yao yamekuwa yakibeba abaria wa aina tofauti.
“Kwa
kweli naipongeza serikali kwa kitendo hiki kwa kuwa abiria wengi wanarudi huku
Njombe na hatujui kama wameathirika au hapana,pia ninashauri juhudi hizi
ziendelee maambukizi haya yatakapofika mwisho”alisema Ndendya
Kelvin
Mwalwanda ni mwenyekiti wa stendi ya mkoa wa Njombe (mji Njombe),amesema
ataendelea kuhakikisha anahamasisha zoezi la kufuata taratibu zote za kujikinga
na virusi hivyo katika stendi ya Njombe.
“Nitahakikisha
ninaendelea kuhamasisha zoezi la kujikinga na Corona linakuwa endelevu na
kuhakikisha kila abaria ana nawa mikono kwa kuwa unapojikinga wewe maana yake
unamkinga mwingine”alisema Kelvin Mwalanda
Serikali
nchini Tanzania inaendelea na juhudi mbali mbali za kupambana na maambukizi ya
virusi vya Corona (Covid-19) lakini hata hivyo licha jitihada ambazo
zinaendelea hii leo Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Majaliwa
Kasim Majaliwa ametangaza ongezeko la visa vya Corona na kufikia 284 kutoka 254
vilivyotangazwa awali na wizara ya afya huku kati ya hao wagonjwa 256
wakiendelea vizuri,wagonjwa 7 wakiwa kwenye uangalizi wa karibu huku kadhalika wagonjwa 11 wakiwa wamepona
kabisa.
0 Comments