Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Alex Malasusa wa
KKKT Jimbo la Mashariki na Pwani (kushoto), Askofu Mkuu Mwandamizi wa
Jimbo Kuu la Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi (wa pili kushoto),
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zubeir (wa tatu kushoto) na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu (wa nne kushoto) katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na
tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020.
Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipozungumza katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la
ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020
0 Comments