Waliokuwa wasanii wa King’s Music Records, Cheed na Killy wametangaza leo asubuhi kujitoa kwenye lebo hiyo kupitia ujumbe wa pamoja walioweka kwenye kurasa zao Instagram.
Wawili hao wamemshukuru Alikiba pamoja na uongozi mzima wa Kings Music kwa nguvu na sapoti waliyoiwekeza kwao tangu walipoingia kwenye lebo hiyo ya muziki.
“Napenda kuwajulisha fans wangu watu wangu wote waliokuwa wakisupport mziki wangu na wanaoendelea kussuport kazi zangu na hata wasiosupport pia ni kwamba kuanzia leo hii napenda kutamka kuwa mimi sio tena msanii wa King’s Music Records,”ameandika Cheed kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Killy na Cheed ni miongoni mwa wasanii wa awali waliotambulishwa katika lebo hiyo mwanzoni mwa Oktoba 2018.
0 Comments