Kocha wa klabu ya Simba SC, Sven Vandenbroeck amesema kuwa kwa sasa anafikiria timu yake kumaliza mechi zake zote zilizobaki, ndipo itwae ubingwa kuliko kusubiri ubingwa wa mezani.
"Jambo la msingi ni kuona kwamba tunacheza mechi zetu zote, kuliko kufikiria kupewa ubingwa kabla ligi haijaisha"
"Suala la ligi kurejea halipo mikononi mwetu zipo mamlaka husika zinazosimamia ligi" alisema Sven.
Simba ndiyo vinara wa ligi wakiwa na alama 71 baada ya kucheza mechi 28, wakiwa wameshinda mechi 23, wakitoka sare mechi tatu na kupoteza mechi mbili.
Kwa sasa ligi kuu Tanzania Bara imesimama kutokana na mlipuko wa janga la virus vya ugonjwa wa Corona.
Chanzo:Mwanaharakati mzalendo
0 Comments