Na Jackline
Kuwanda, DODOMA
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwelwe
ameshuhudia utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi kwa kiwango cha
lami,Barabara ya Mzunguko ya jiji la Dodoma ya njia nne ambayo ina kilomita
112.3 unaofadhiliwa na Benki ya Afrika.
Mradi huo unatekelezwa na serikali kwa gharama ya
Bilioni mia nne na tisini na nne (494) ambapo shilingi Bililoni mia nne kumi na
mbili (412) ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika
na shilingi Bilioni themanini na mbili (82) ni mchango wa serikali
ya Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiliaji saini
wa wa mradi huo, Mhandisi Kamwelwe amesema Mradi pia utahusisha miradi mingine
midogo midogo katika maeneo ya jiji la Dodoma huku akisema ni matarajio yake
kuwa mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa.
Wakati huo amesema ujenzi wa mradi huo utakapo anza
itakuwa ni fursa ya ajira kwa watanzania na wachangamkie fursa hiyo hasa wakazi
wa Dodoma huku akiwataka wale ambao watapata fursa ya kufanya kazi katika mradi
huo kuwa walinzi wa mali zote za mradi na kujiepusha na wizi wa vifaa.
Akitoa Taarifa fupi ya ujenzi wa Barabara ya njia
nne kuzunguka jiji la Dodoma, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick
Mfugale amesema Barabara hiyo ina urefu wa kilomita 112.3 na imegawanywa katika
maeneo mawili ili kusudi ujenzi huo uweze kukamilika kwa muda.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Bilith
Mahenge amesema mradi huo ni kati ya mradi utakao changia kuifanya Dodoma kuwa
ya kisasa iliyojengwa kwa kutumia Sayansi ya Tekinolojia ikiwa na maana ya
kwamba jiji la Dodoma litawezeshwa kuwa jiji linalo vutia.
Mradio huo kama ilivyo miradi mingine utajumuisha
miradi midogo midogo inayogusa jamii kwa pamoja katika sekta za Afya,
Maji,Elimu hata Barabara na usalama Barabarani.
0 Comments