Na Amiri Kilagalila,Njombe
Pamoja na juhudi za wakala wa maji safi na usafi wa
mazingira vijijini (RUWASA) na serikali
ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe
katika kuhakikisha huduma ya maji safi na salama yenye kutosheleza
inawafikia wananchi wote.
Bado kuna changamoto katika usimamizi na uboreshaji
wa miradi iliyopo na inayoendelezwa ili kuongeza huduma endelevu kwa jamii ya
wilaya hiyo.
Amebainisha hilo kaimu meneja RUWASA wilaya ya
Wanging’ombe Inj.Charles Mengo katika mkutano mkuu wa wilaya kwa jumuiya za
maji uliofanyika wilayani humo huku
akieleza njia mbali mbali zitakazoweza kukabiliana na changamoto hiyo kwa jamii
ikiwemo mikutano ya pamoja ya mara kwa mara ya jumuiya za watumia maji.
“Ili kubolesha na kuongeza ufanisi katika utoaji wa
huduma hiyo,ni lazima kuendelea kuwepo
na mkutano mkuu wa wilaya mara mbili kwa mwaka kwa ajili ya kujadili
chanagamoto hizo katika utoaji wa huduma utakao wakutanisha wataalamu wa
maji,kamati za maji pamoja na watumishi wa jumuiya za maji ili
kujadili,kutathmini na kubadilishana uzoefu katika maswala mbali mbali
yanayohusu maji na usafi wa mazingira”alisema Inj.Charles Mengo
Aidha amesema hali ya huduma ya maji katika wilaya hiyo
ina jumla ya miradi ya maji 36 inayotumia tekinolojia mbali mbali huku visima
vifupi 443,virefu 12 ikiwa ni pamoja na mabwawa madogo madogo.
Vile vile amesema huduma ya maji safi na salama
inawafikia wakazi wapatao laki moja hamsini elfu na mia sita themanini na
sita (150,686) kati ya wakazi hao wakazi
wapatao stini na tatu elfu na tisini na tatu sawa na 71% ni wa maeneo ya vijijini na wakazi wapatao
85,393 sawa na asilimia 88.42 ni kwa maeneo ya mjini.
Veronicka Gelad ni kaimu katibu tawala wilaya ya
Wanging’ombe,ametoa wito kwa jumuiya za maji kuweka mikakati madhubuti
itakayosaidia kuhakikisha miundombinu ya maji inatunzwa.
“Katika kukabiliana na changamoto zinazoathiri
uendeshaji wa miradi ya maji vijini
ambayo serikali inatumia fedha nyingi,ni lazima tujitoe kwa kuchangia ghalama
za kuchangia miradi yetu ya maji hivyo kila mmoja ni lazima awe barozi,ninaamini
wanajumuiya kuweka mikakati madhubuti ambayo itasaidia wanajumuiya na jamii
kuhakikisha miundombinu ya maji inatunzwa na maji yanapatikana kwa
wakati”alisema Veronicka
Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa jumuiya za
watumia maji,wamesema ipo haja ya kuendelea kushirikiana na jamii kikamilifu
ili kusaidia utunzaji wa vyanzo vya maji huku wakiomba wakala wa barabara
mijini na vijijini TARURA wilayani humo kuwa na ushirikiano na jumuiya za
watumia maji ili kukabiliana kwa pamoja na uharibu wa miundombinu ya maji
zinapotengenezwa barabara.
Simon Msemwa,Tumain Sanga na Roda Ngimbudzi ni
wakazi wa kijiji cha Itulahumba wanaonufaika
na uwepo mradi wa maji uliopo kijiji jilani cha Isindagosi ambao ni miongoni
mwa miradi mikubwa ya maji wilayani humo.wamesema licha ya uwepo wa changamoto
kwa baadhi ya miradi wanaomba jamii kuendelea kutunza vyanzo vya maji huku wakishukuru
kupata maji karibu na makazi yao.
0 Comments