Na Omary Mngindo, Yombo
HALMASHAURI ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imepeleka kiasi cha shilingi milioni 60 katika Kituo cha afya Kata ya Yombo, kinachojengwa Kijiji cha Matimbwa wilayani hapa, ili kianze kuwapati huduma wananchi.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ally Ally, mbele ya Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, iliyotembelea Kituo hicho hivi karibuni ambapo lengo ni kuharakisha upatikanaji wa huduma ya afya katani humo.
Ally alisema kwamba, wakati wanasubiri fedha kutoka serikali Kuu kiasi cha shilingi milioni 200, halmashauri imepeleka kiasi hicho, ambapo washanunua vitanda, huku kiasi kingine kikienda katika madawa ili huduma zianze mara moja.
"Mwenyekiti kama unavyofahamu, Kituo hiki tumepatiwa shilingi milioni 400, nasi kama halmashauri tukaona wakati Serikali Kuu ikiwa na mpango wa kutupatia shilingi milioni 200, kwa kuona zinachelewa tumeleta shilingi milioni 60 kwa ajili ya vifaa tiba, "alisema Ally.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa halmashauri Mohemed Usinga ambaye ndio Diwani wa Kata, ameiomba Kamati hiyo kufuatilia taarifa za mradi huo, zilizoshikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), huku kukiwa hakuna taarifa zozote.
"Tunaitambua TAKUKURU ni taasisi ya Serikali inayofanyakazi zake kisheria, lakini tusikitishwa kwa kitendo cha taarifa ya mradi huu kuchukua kwa muda mrefu, pasipo wao kupatiwa taarifa ya nini kinaendele, tunaiomba Kamati kukutana na wakubwa wenzenu kuzungumzia hili," alisema Usinga.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya ujenzi hyo na maelezo ya Madiwani hao, Abdul Sharifu, alisema kuwa wao wanamwakilisha Mwenyekiti wa (CCM) Taifa Dkt. John Magufuli, hivyo taarifa za kuchelewa kwa fedha hizo watazifikisha kwa viongozi husika, ili hatua za haraka zichukuliwe.
"Niwapongeze Halmashauri kwa hatua mliyoichukua cha kuleta fedha hizo ili Kituo hiki kianze kazi, DMO natoa wiki mbili kuanzia leo, kituo hiki kianze kuwahudumia wannchi, namimi hiyo siku nitakuwa mmojawapo wa wataohudumiwa," alimalizia Sharifu.
0 Comments