TANGAZA NASI

header ads

KM ARDHI AWATAKA WATHIMINI MALI KUTOGEUZA OFISI SEHEMU YA UPIGAJI WA FEDHA KWA WANYONGE

 


NA TIGANYA VINCENT

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo amewataka Wathamini mali kutogeuza Ofisi sehemu kuwashawishi kupata fedha kutoka kwa wananchi wanyonge.

Alisema vitendo vya aina hiyo vinaacha mauvimu kwa wananchi wanyonge na kufanya walie machozi  ya uchungu baada ya kupewa thamani ndogo ya mali zao na kulipwa fidia kidogo ya kiasi anachotakiwa kupata.

Mary alitoa kauli hiyo jana mjini Tabora wakati akifunga mafunzo ya siku 12 kwa Wathamini mali 72 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.
“Nendeni mkafanye kazi msigueze Ofisini zenu kuwa sehemu ya kufanyia consultation kwa ajili ya kutaka kuwakandamizi wanyonge kwa kuwatoza fedha…Serikali inakulipa fedha kwa nini wewe usiwatumike wananchi…kuweni na huruma kwani mwananchi unayemdhulumu haki …machozi yake yupo  atakayemfuta na machozi hayo yatakuandama wewe na kizazi chako chote” alisisititiza.

Alisema baadhi ya Wathamini wasio waaminifu wamekuwa wakifanya tathimini ya mali za wananchi wanyonge kwa kiwango cha chini kwa ajili ya kuwakandamizakwa lengo kutaka kuwashiwishi wawepe rushwa.

Mary aliongoza kuwa wapo baadhi yao wamekuwa wakitathimini kwa kuongeza na wengine kupunguza thamani ya mali tofauti na hali halisi kwa maslahi binafsi na kuisababishia Serikali hasara kubwa.

Alisema wapo baadhi ya Wathamini wanashirikiana na watumishi wa Taasisi za fedha kufanya tathimini mali hewa ikiwemo kuonyesha uwepo wa nyumba wakati haipo na kusababisha hasara kwa Taasisi hizo.

Mary alisema kuwa baadhi yao wamekuwa wakichelewesha kwa makusudi kazi za uthamini bila sababu kwa lengo kuweka mazingira ya kushawishi kupewa rushwa.

Katibu Mkuu huyo aliitaka Bodi ya Wathamini kuwachukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kuwanyang’anya leseni za ufanyakazi Wathamini ambao watabainika kukiuka maadili ambao utafanya taalumu hiyo kushuka hadhi katika jamii.

Aidha Mary aliwataka wahitimu hao wa Utathimini kufungua ukurasa upya na kufanya jamii kuwaamini kwa kutenda kazi zao kwa uadilifu na uzalendo zaidi.

Mtathimini kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali Baraka Molleli alisema kuswa baada ya mafunzo hayo watakwenda kuwa kioo kwa wafanyakazi wenzake.

Post a Comment

0 Comments