TANGAZA NASI

header ads

Familia ya Filikunjombe yasherehekea Eid na Wafungwa Pamoja na Mahabusu Ludewa



Na Nickson Mahundi


Katika kusherekea sherehe ya Eid AL FITR familia ya Filikunjombe iliungana na wanafamilia wa Gereza la kilimo la Ludewa(gereza la Ibihi) katika chakula cha pamoja na wafungwa ,mahabusu Pamoja na familia za Askari wa gereza hilo. 


 Familia ya Filikunjombe imetoa Ng'ombe mmoja ambaye amechinjwa katika sikukuu ya Eid Pamoja na mchele, soda, maji namahitaji mengine .



Akipokea vitu hivyo mkuu wa gereza hilo SP Joannes Baitange Alisema kuwa ni watu wachache Sana wanaowakumbuka wafungwa hivyo ameishukuru familia ya Filikunjombe kulikumbuka gereza hasa katika sikukuu Kama ya leo. 



Hata hivyo SP Baitenge aliiomba familia hiyo ambayo iliwakilishwa na Dr Philip Filikunjombe katika chakula na wafungwa kuendelea kulikumbuka wafungwa na mahabusu katika gereza hilo hasakatika utatuzi wa changamoto nyingine ikiwa na computer na printer ambavyo Kwa sasa vinahitajika sana. 



Aidha Dr Filikunjombe alisema kuwa ni utaratibu wa familia yao kulitembelea gereza hilo kwani tokea kaka yake hayati Deo Filikunjombe ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa ndiye aliyeanzisha utaratibu huo hivyo yeye na ndugu zake wanaendeleza utaratibu huo. 



"tumekuwa tukifanya haya Kwa muda sasa kwa kutoa nahitaji mbalimbali hapa gerezani ikiwa nikuwafariji wafungwa na mahabusu hii ni sadaka yakifamilia ambayo tumejiwekea utaratibu huu na tunauendeleza kila mwaka ",alisema Dr. Filikunjombe.

Post a Comment

0 Comments