TANGAZA NASI

header ads

Utapiamlo mkali wapungua kwa watoto mjini Makambako




NA BILGITHER NYONI


Hali ya utapiamlo mkali kwa watoto katika halmashauri ya makambako mkoani Njombe imetajwa kupungua baada ya serikali kuandaa mikakati mbali mbali na kupambana na tatizo hilo.


Hayo yamesemwa na Afisa Lishe wa Halmashauri ya mji wa Makambako SALMA ABDALAH wakati akizungumza na waandishi ofisini kwake ambapo amesema kuwa kwa sasa katika wodi ya kulaza watoto wenye Lishe duni hakuna mgonjwa yoyote lakini wanaendelea na mpango wa kutoa elimu ya lishe kwa wazazi ili kuendelea kupambana na tatizo hilo.


``kwa sasa hali ya watoto wenye utapiamlo mkali imepungua kwa kiasi kikubwa kwa sasabu kama  unavyoona hapa wodini kwetu hakuna mteja hata mmoja aliyelazwa kwenye wodi yetu na hii inapata kama wiki ya pili sasa,kitu ambacho tunakifanya ni huduma tunazozitoa hapa kwa sababu tuna maziwa ya dawa ambapo mtoto akija hapa anaanzishwa ``Amesema Bi Salma. 


Veronika Mutobe ni Muuguzi anayehudumia wodi ya watoto wenye lishe duni ambaye amesema mara nyingi watoto wenye matatizo ya utapia mlo huathirika kutokana na baadhi ya wazazi kutumia muda mwingi kufanya shughuli za kibiashara na wakiwaacha watoto bila lishe bora Hivyo amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanawapa lishe bora.


``huu ni mji wa kibiashara kinamama wengi baadhi yao hawazingatii maswala  ya lishe wakati fulani watoto wanaenda shule bila hata kupata chakuala, mpango wetu ni kuendelea kuafikia kinamama kwenye maeneo yao ya kazi ili kuwa elimu ya lishe``Amesema Mutobe


Aidha Mutobe amekumbusha kuwa lishe ya mtoto inaanza tangu mtoto anapokuwa tumboni hivyo amewataka Wazazi kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya kwa kuhudhuria klinik mapema na kula chakula bora.


Nao baadhi ya kinamama mjini makambako wamekiri kupata elimu ya Lishe kila wanapohudhuria kliniki na kuahidi kufanyia kazi ushauri wanaopewa na wataalamu ili kuwakinga watoto wao na utapia mlo.


Mikakati mbalimbali imewekwa na halmashauri katika  kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa wanajamii .



Post a Comment

0 Comments