TANGAZA NASI

header ads

Mkalimani afunguka "Niliongea mengi mmeliona lile"

 


Mkalimani Matungwa Mutatina aliyezua gumzo mitandaoni siku ya kumuaga Hayati Dkt John Pombe Magufuli Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, amesema kilichomtokea sio kushindwa kutafsiri maneno bali ni matatizo ya kiufundi.


Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Mkalimani huyo amesema mitambo ilifika mahala ambapo sauti inatoka ikiwa inakatakata kisha akawa hasikii kabisa sauti inayotoka kwa aliyekuwa anaongea.


"Ile hali ilinistua kidogo, kilichokuwa kimetokea haikuwa kwamba nimeshindwa kutafsiri maneno ila kulikuwa na sababu za kiufundi, mitambo ilifika mahala ikawa haisikii na sauti inakuja kwa kukatakata lakini haikunivunja moyo, kwa sababu waliokuwa wanacheka hawakujua kilichotokea na kuendelea" ameeleza Mkalimani Matungwa Mutatina 


Aidha Mkalimani amesema anawaomba watu wawe na uzalendo na wajirekibishe kwa kilichotokea kwa sababu kulikuwa na vitu vingi hasa ilikuwa siku ya kumuaga Hayati Dkt John Pombe Magufuli ila watu wamemdhihaki na kumcheka kwa kilichomtokea.

Post a Comment

0 Comments