TANGAZA NASI

header ads

Polisi yazuia shamrashamra Pasaka

 


Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Pasaka kama za kipindi cha nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.


Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime, imeeleza kuwa endapo kila mwananchi atazingatia na kufuata sheria na kujiepusha na vitendo vya uhalifu Ibada na Sikukuu ya  Pasaka zitamalizika salama.


Amesema Jeshi la Polisi limejipanga vizuri katika kuhakikisha waumini wanashiriki ibada za Pasaka makanisani katika mazingira ya  amani, salama na utulivu na wannachi wengine kuendelea na shughuli zao kama kawaida.


Aidha Jeshi la polisi limetoa wito kwa Kamati za Ulinzi na Usalama katika nyumba za ibada na sehemu zingine kushirikiana katika kudumisha amani, utulivu na usalama.



Post a Comment

0 Comments