TANGAZA NASI

header ads

Chadema kutoshiriki uchaguzi wa ubunge Muhambwe

 


Chama cha Chadema kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Muhambwe lililopo wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma.

Jimbo la Muhambwe liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge Atashasta Nditiye kufariki dunia Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari iliyotokea Februari 10, 2021 eneo la Nane Nane, mkoani humo.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 naibu katibu mkuu wa Chadema, Benson Kigaila amesema baada ya kikao cha kamati kuu kilichofanyika Machi 31, 2021  kwa njia ya mtandao wameazimia kutoshiriki uchaguzi huo kutokana na mazingira ya tume ya uchaguzi kutotenda haki.


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshatangaza kuwa uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika Mei 2, 2021.


Tayari Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Florence Samizi kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.


Post a Comment

0 Comments