TANGAZA NASI

header ads

Msaidizi wa Merkel aonya kuhusu hatari ya kushindwa kudhibitiwa kwa Covid-19 Ujerumani

 


Msaidizi mwandamizi wa Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Helge Braun amesema Ujerumani lazima ipunguze kiwango cha maambukizi ya virusi vya corona katika majuma machache yajayo vinginevyo itajiweka katika hatari ya kuibuka virusi vipya ambavyo ni sugu kwa chanjo.


Na vilevile amesema kuwekwe marufuku ya kutotoka nje katika nyakati za usiku katika majimbo ambayo yana kiwango kikubwa cha visa vya maambukizi hivyo.


Akizungumza na gazeti la kila Jumapili la Ujerumani la Bild am Sonntag, Braun amesema Ujerumani kwa sasa ipo katika kipindi cha hatari zaidi cha janga la virusi vya corona. 


Na kwamba katika wiki chache zijazo itaweza kufahamika kama janga hilo limeweza kudhibitiwa au la.Kwa mujibu wa taarifa ya Jumamosi ya taasisi ya Robert Koch idadi ya maambukizi nchini Ujerumani imeongezeka kwa watu 20,472 wakati vifo vilivyoongezea ni 157.

Post a Comment

0 Comments