TANGAZA NASI

header ads

Wanamgambo wauteka mji wa kaskazini mwa Msumbiji

 


Kundi la wapiganaji la wenye itikadi kali limeudhibiti wa mji mmoja kaskazini mwa Msumbiji na kuwaua watu kadhaa akiwemo mfanyakazi mmoja wa kigeni, na kuilazimisha kampuni kubwa ya mafuta ya Ufaransa, Total kusitisha shughuli zake katika mradi mkubwa wa gesi.


Duru za usalama zimesema jana kuwa wanamgambo hao walianza kuushambulia mji wa Palma katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado siku ya Jumatano na kuwalazimisha takriban watu 200 wanaowajumuisha wafanyakazi wa kigeni wa mradi huo wa gesi kutoka katika hoteli waliokuwa wamejificha. 


Shambulio hilo linafanyika muda mfupi baada ya kampuni ya Total kutangaza kuwa itaanza kurejelea pole pole shughuli zake katika eneo hilo ambazo zilikuwa zimesitishwa kufuatia mashambulio ya awali. Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa kiasi cha wafanyakazi saba waliuawa katika ghasia za hivi karibuni ikiwa ni pamoja na raia mmoja wa Afrika Kusini.

Post a Comment

0 Comments