TANGAZA NASI

header ads

MAPINDUZI BALAMA, DICKSON JOB KAMILI GADO KWA KAZI YANGA



 KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa maendeleo ya nyota wake ambao walikuwa wakisumbuliwa na majeraha ikiwa ni pamoja na Mapinduzi Balama, Dickson Job yamezidi kuimarika.

Job alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja ambayo aliyapata kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ila kwa sasa amerejea kwenye ubora wake na kuanza mazoezi.

Balama alikuwa nje kwa muda mrefu akitibu majeraha ya kisigino aliyoyapata msimu wa 2019/20 aliyoyapata kwenye mazoezi ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara ilikuwa dhidi ya Ndanda FC.

Tayari naye ameanza kupewa program maalumu ambayo itaweza kumrejesha uwanjani kuendelea na majukumu yake.

Mwambusi amesema:"Kila mchezaji anaonekana kuwa na furaha na taratibu wale ambao hawakuwa fiti wanarudi, Mapinduzi Balama amepewa program maalum huku wachezaji wengine wakiwa wameanza mazoezi.

"Fiston naye kwa sasa anaendelea vizuri ni jambo jema kwetu na tunaamini wale wengine ambao hawajawa kwenye ubora wataimarika," .

Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 23 inafuatiwa na Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ipo nafasi ya pili na pointi 46 baada ya kucheza mechi 20.

Imeanza mazoezi ikiwa na nyota wake ambao ni pamoja na Paul Godfrey, Yacouba Songne, Ramadhan Kabwili, Kibwana Shomari.

Post a Comment

0 Comments