Na.Catherine Sungura.WAMJW,Dodoma
Serikali imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya unakuwa wa kuridhisha.
Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wizara (Idara Kuu ya Afya) kwa kipindi Cha Julai 2020 Hadi Februari,2021 Kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii jijini Dodoma.
Dkt.Gwajima amesema katika kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana kwa wakati na zenye ubora,Serikali ilitenga kiasi Cha shilingi Bilioni 200 katika kipindi Cha mwaka 2020/2021 kwa ajili ya ununuzi wa dawa,vifaa,vifaa tiba na vitendanishi.
Aidha,Dkt. Gwajima amesema upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa aina 312 za Dawa upatikanaji umefikia kiasi Cha asilimia 74.
0 Comments