Na Timothy Itembe Mara.
KUNDI namba tatu la waandishi wa habari walioshiriki semina ya siku tatu iliyoandaliwa na Kituo cha sheria na haki za Binadamu(LHRC) juu ya kuandika habari za changamoto ya migogoro na utatuzi wake semina iliyofawashirikisha waandishi kutoka Pwani,Mtwara na Mara ambapo kundi hilo limekuja na mwaarobaini wa migogoro ya kusambaratika kwa ndoa.
Wakijadili katika semina iliyofanyika Dare-salamu wiki iliyopita kundi hilo lilisema kuwa ili ndoa ziendelee kudumu kuna haja wanandoa kukaa pamoja na kujadili matatizo yanayowakabili ikishindikana washirikishe jamaa ndugu na marafiki.
Kundi hilo kwa pamoja walisema kuwa kuna haja wanandoa kukaa pamoja katika meza moja wakitatua changamoto zinazowakabili ikishindikana watafute suluhu nje ya hapo.
Naye Afisa Vijana wa kituo cha sheria na haki za Bianadamu(LHRC
)Ally Seif Ramadhani alisema kuwa lengo la kunda makundi kwenye semina iliyowashirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Pwani,Mtwara na Mara ni kujenga uzoefu wa kuandika habari za migogoro na changa,moto zake bila kaudhiri pande mbili zaianzo hasimiana.
Afisa huyo aliongeza kusema baadhi ya migogoro inaibuka kwa nje ikionekana midogo kumbe ndani yake mizizi mirefu sana imejificha jambo ambalo linatakiwa kwenda kwa umakini katika kuandika na kutafuta suluhu.Akitolea mfano Binti mjasilia mali wa kuuza viatu ambaye hakutaja jina lake mwenye umri wa miaka 20 kudai kubakwa na mteja wake ambaye waliounganishwa kwa njia ya Fece book alisema aliingilia kati mgogoro huo kumbe ndani yake kuna sontofahamu.
“Mimi niseme kuwa waandishi wa habari na wale wote ambao wanahusika katika kutatua migogoro mbalimbali kwenye jamii kuna haja wawe makini katika kutatua,akitolea mfano binti mjasilia mali wa kuuza viatu wa miaka 20 ambaye alidai kubakwa nahuyo mteje wake alisema aliingilia huo mgogoro kumbe alikuwa amedanganywa baada ya Binti huyo kuulizwa maswalai mengi ilibainika kuwa kijana huyo alikuwa mpenzi wake ila walitofautiana masilahi ”alisema Ramadhani.
Ramadhani alimaliza kusema kuwa kuna hatua nyingi za migogoro katika kuzitatua ambapo katika hilo kunahitajika umakini wa hali ya juu kusuluhisha mgogoro pasipo kupendelea upande wowote ili mwisho wa siku maridhiano ya Amani yapatikane.
Kwa upande wa Calorine Shoo ambaye ni mratibu wa mradi wa Jenga Amani Yetu alisema kuwa waandishi wa habari kutoka mikoa mitatu ya Tanzania Bara wameshirikishwa katika semina hiyo wakati huo huo ukitekelezwa huko Zanzibar.
Kituo cha sheria na haki za binadamu kimekuja na mradi wa Jenga Amani Yetu ni mradi unaofanywa na kituo cha sheria na haki za binadamu(LHRC),Zanzibar Legal Service Center(ZLSC) pamoja na Search for Common Graund(SFCG) kwa ufadhili wa Jumuya ya Ulaya( EU) alisema Shoo.
Kila moja anapaswa kujiona ni sehemu ya kujenga Amani,nivigumu kuepuka migogoro lakini tunaweze kuepuka vurugu katika jamii zetu aliongeza kusema Shoo.
Wakichangia baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walitumia nafasi hiyo kushukuru Kituo cha sheria na haki za binadamu kuandaa mafunzo hayo ambapo waliongeza kuwa elimu waliyoipata imeongeza mbinu mbalimbali za kuandika habari za kutatua changamoto za migogoro.
Frankius Cleophace Mara alisema kuwa mafunzo aliyoyapata juu ya migogoro na namna ya kuishugulikia kwa lengo la kupata suluhu itamuongezea weledi.
Mwanahabari huyo alitumia nafsi hiyo kupongeza kituo cha sheria na haki za binadamu kuleta mafunzo hayo lengo ni kutaka Nchi ya Tanzania kuwa na Amani kwa maendeleo ya wananchi wake.
Kundi namba tatu waja na mwaarobaini kusambaratika kwa ndoa.
0 Comments