NA,SALVATORY NTANDU
Wazazi
na Walezi Mkoani Shinyanga wametakiwa kuchukua tahadhari kwa watoto wao
dhidi ya wanyama aina ya Fisi ambao wamekuwa wakionekana katika maeneo
mbalimbali na kusababisha madhara kwao ikiwemo ya vifo.
Kauli
hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora
Magiligimba June 2 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na
tukio la kushambuliwa hadi kufariki dunia kwa mtoto wa miaka miwili na
nusu aliyehamika kwa jina la Charles Christian katika kitongoji cha
Mwagala kata ya Ibadakuli.
Amesema
tukio hilo limetokea June Mosi mwaka huu majira ya saa moja usiku akiwa
anacheza na watoto wenzake nje ya nyumba yao alijeruhiwa kwa kung'atwa
na fisi sehemu za usoni na kisha kuburuzwa umbali wa mita 50 ndipo
wananchi walipoamua kumfukuza akamuachia na kukimbia baada ya kuzidi kwa
kelele za wananchi hao.
“Wanyama
hawa wamekuwa wakizurura ovyo hivyo ni Budi kila mzazi /Mlezi
kuhakikisha watoto wao wanakuwa salama na kwani matukio ya watu
kushambuliwa na fisi ama mifugo yamekuwa ni mengi hivyo chukueni
Tahadhari,”alisema Magiligimba.
Amefafanua
kuwa Charles alifariki dunia akiwa njiani akisafirishwa kwenda katika
hospitali ya rufaa ya kanda ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu na
mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga
kwaajili ya kukabidhiwa ndugu zake kwaajili ya Matibabu.


0 Comments