Aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha
Redio cha Clouds FM Hamis Mandi maarufu B Dozen amejiunga na Kituo cha redio
cha EFM- Tanzania
Mandi ambaye anafahamika zaidi kwa
jina la utangazaji la B-Dozen (The Navigator, Msafiri) kwa muda mrefu alikuwa
akiongoza kipindi cha XXL cha Clouds FM, pamoja na vingine.
Kupitia ukurasa wao wa Instagram,
E-FM wameandika mbobezi huyo wa utangazaji amejiunga nao, na kwamba
kinachofuata ni kupaa juu, na kuhakikisha mafanikio zaidi kwa Tanzania.


0 Comments