BAADA ya kupewa dili la miezi mitatu kuinoa Klabu ya yanga, kocha mpya wa makipa Razak Siwa amesema kuwa anaamini atafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Kocha huyo raia wa Kenya alitambulishwa rasmi jana, Machi 29 na tayari ameanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kinachosimamiwa na Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi.
Mwambusi amechukua mikoba ya Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7,2021 kutokana na matokeo mabovu kwa mujibu wa mabosi wa Yanga ambapo mzunguko wa pili kwenye mechi 6 alishinda moja na kuambulia kichapo moja huku nne akiambulia sare.
Nizar Khalfan ambaye alikuwa msaidizi wake naye alifutwa kazi huku kocha wa makipa Niyonkuru raia wa Burundi naye akichimbishwa na nafasi yake imechukuliwa na Siwa.
Siwa amesema:"Nimefurahi kuwa hapa na nitatoa ushirikiano mkubwa na kila mchezaji pamoja na uongozi kiujumla," .
0 Comments