TANGAZA NASI

header ads

Klabu ya Manchester City Yathibitisha Mchezaji Sergio Aguero Kuondoka Katika Klabu Hiyo

 


Klabu ya Manchester City imetangaza kuwa mshambuliaji wao Sergio Aguero ataondoka klabuni hapo mkataba wake utakapomalizika majira ya kiangazi mwaka huu.


Mshambualiaji huyo raia wa Argentina alijiunga na Man City mwaka 2011 na kuiwezesha kushinda ubingwa wa Premiere League kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 44. Katika kipindi chote Aguero amefunga mabao 257 kwenye michezo 384 akiwa na Man City.



Post a Comment

0 Comments