TANGAZA NASI

header ads

Klabu ya Simba kumtangaza kocha mkuu kesho



 Klabu ya soka ya Simba imethibitisha kwamba inatarajia kumtangaza kocha mkuu wa kikosi hicho kesho Januari 23 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbra Gonzalez ambaye ameyasema hayo wakati akitambulisha mashindano yao mapya yajulikanayo Simba Super Cup yanayotarajiwa kuanza Januari 27 hadi 31 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Akizungumzia juu ya mashindano hayo, Barbra amesema wanatarajia kocha atakayetangazwa kesho ndiye atakayeiongoza Simba katika mashindano ya Super Cup wiki ijayo, ambapo itapepetana dhidi ya vilabu vya Tp Mazembe ya DR Congo na Al Hilal ya Sudan .

''Tunatarajia kumtangaza Kocha mpya kesho, ndiye atakayeiongoza timu yetu katika michuano ya Simba Super Cup, haya ni mashindano mapya na yatatusaidia kuiandaa timu na ligi ya mabingwa Afrika'' Alisema Barbra.

Simba imepangwa kundi A la ligi ya mabingwa Afrika ambapo itaumana na vilabu vya AS Vita, Al Ahly na Al Merrikh, michuano inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Februari 14 mwaka huu.

Katika htua nyingine, Barbra amesema kwamba mshambuliaji wao Benard Morrison amepona maradhi yaliyokuwa yakimkabili na anatarajiwa kushiriki katika michuano ya Simba Super Cup.

Post a Comment

0 Comments