Na Amiri Kilagalila,Njombe
Rainary Lugome mkazi wa wilaya ya Ludewa mkoani
Njombe ameuawa na ndugu yake aliyefahamika kwa jina la Claus Samweli Lugome
(46) kwa tuhuma ya kuku wake kuingia katika shamba la kaka yake.
Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa polisi
mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema wanawashikilia wanafamilia wawili akiwemo
baba wa watoto hao Ado Samweli Lugome pamoja na kijana aliyehusika na mauaji
kwa ajili ya upelelezi.
“Haya mauaji ni ya hovyo,yaani kaka kamuua mdogo
wake kisa na mkasa kuku wa mdogo mtu wameenda kwenye shamba la kaka mtu”alisema
Kamanda Issa
Hata hivyo ameongeza kuwa katika upelelezi uliokuwa
unaendelea wamebaini familia hizo zimekuwa zikituhumiana na maswala ya
ushirikina.
“katika ufuatiliaji wa swala hili tumeona
wanatuhumiana kuwa mmoja anatembea na mke wake na mwingine anamtuhumu mwenzie
kuwa alikuwa anamloga”alisema kamanda
Ametoa rai kwa jamii kuacha kuamini ushirikina
badala yake kutoa taarifa sehemu husika ili kusaidiwa kuliko kuchukua hatua
mkononi.
0 Comments