Mchungaji wa kanisa la Pentecostal Gospel mission (PGM), Boston Chimalilo (72) mkazi wa wilaya ya Mbinga anashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kumnajisi mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 13.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Desemba 4, 2020 kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa amesema alikamatwa eneo la makaburini Desemba mosi, 2020 akijiandaa kumwingilia mwanafunzi huyo.
Amesema mchungaji huyo alikutwa akiwa amepiga magoti na alipobaini kuwa ameonekana alianza kukimbia lakini wananchi walimkamata pamoja na mwanafunzi huyo na kuwapeleka polisi.
Amesema mwanafunzi huyo alipohojiwa alikiri kuwa na mahusiano na mchungaji huyo tangu mwaka 2019.
Kamanda huyo amebainisha kuwa uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea na kwamba mchungaji huyo anatuhumiwa pia kuwarubuni wanafunzi wengine watatu lakini walikataa, “upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.”
0 Comments