Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Diwani pekee kupitia
Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kutoka kata ya Uhenga kati ya
madiwani 28 wa halmashauri ya wilaya ya
Wanging'ombe mkoani Njombe ameapishwa pamoja na madiwani wengine wa Chama cha
Mapinduzi licha ya Chama chake kuendelea na msimamo wa kuto tambua madiwani na
mbunge walioshinda katika nafasi hizo kwa madai ya uchaguzi uliopita kuto kuwa
wa huru na haki.
Katika kikao Cha
kwanza Cha Baraza maalamu la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe
kilichofanya kazi ya Kuwaapisha madiwani hao,Kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa
Halmashauri na Makamu wake pamoja na Kamati mbalimbali kimewachagua pia Agnetha
Mpangile Diwani wa kata ya Ulembwe kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu
wake Onesmo Lyandala ambaye Ni Diwani wa kata ya Imalinyi Huku Hakimu mkazi
mahakama ya mwanzo Makambako na Mdandu Almachius Kasaizi Wakati akiwaapisha
amewataka kwenda kukitumikia kiapo.
“Majukumu mnayoenda
kuyafanya ni kuyatekekeleza kwa mujibu wa sheria,uadilifu na uaminifu” alisema Almachius
Kasaizi hakimu mkazi mahakama ya mwanzo Makambako na Mdandu wakati akiwaapisha
madiwani
Chadema kupitia Kamati
kuu kilitangaza kutotambua madiwani na mbunge walioshinda nafasi zao kwenye
uchaguzi mkuu wa October 28 mwaka huu huku Diwani wa kata ya Uhenga bwana Alfan
Kawambwa amekula kiapo kwa madai ya kuto
kuwa na barua ya kumzuia kwenda
kuapishwa.
“Kutokana na matamkoa mbali mbali ya Chama changu,sina
barua rasmi ya kunizuia kuja kuapa,kwa hiyo nimekuja kuapa nikiwa na baraka
zote kama diwani wa kata ya Uhenga,Nimeingia ukumbini mpaka ninaapa sikuwa na
barua yeyote inanizuia nisile kiapo cha uaminifu kama diwani wa kata ya Uhenga”Alisema
Alfan Kawambwa
Baadhi ya madiwani
kupitia Chama Cha mapinduzi CCM akiwemo Thobias Mkane Annaupendo Gombela na
Syrevester Kigora Wamesema hata Kama Halmashauri hiyo imempata Diwani
Mmoja toka Chadema lakini wanaamini kuwa Hali itakuwa shwari kwa kuwa lengo Lao
Wote Ni kuwaletea maendeleo Wananchi.
“Kuwepo
mwenzetu wa upinzani hili halitaathiri hata sehemu moja utendaji wa kazi za
halmashauri kwasababu tutafanya kazi kwa mujibu wa miongozo ya serikali na
tunachoaidi sisi ni maendeleo kwa wananchi”alisema Thobias Mkane
Siku chache zilizopita mwandishi wetu alizungumza na
mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Rose Mayemba, juu ya
taarifa za madiwani wake kwenda kuapishwa ambapo alisisitiza msimamo wa Chama
hicho kwa madiwani wao wa kata 4 waliochaguliwa mkoani humo kuendelea
kuzingatia utaratibu huku akieleza kuchukuliwa hatua watakapokiuka utaratibu.
“Kama ambavyo katibu mkuu wa Chama chetu
alivyozungumza juu ya wote walioshinda kwenye nafasi zao Chama hakijabadirika
bado kwamba hawatambuliwi wabunge na hawatambuliwi madiwani” Alisema Rose
Mayemba
0 Comments