TANGAZA NASI

header ads

Mfalme wa Kuweit amteuwa tena Sheikh Sabah al-Khalid kuwa waziri mkuu

 


Mfalme wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad al-Sabah amemteua tena Sheikh Sabah al-Khalid al-Sabah kuwa waziri mkuu wa taifa hilo, baada ya uchaguzi wa bunge wa taifa hilo la Ghuba, linalokabiliwa na hali mbaya kabisa ya kiuchumi. 

Sheikh Nawaf amemtaka Sheikh Sabah kuteuwa baraza la mawaziri ili lipatiwe idhini. Hata hivyo wachambuzi wanasema muundo wa bunge jipya unaweza kutatiza jitihada za mabadiliko za serikali katika kushughulikia ukwasi katika taifa hilo ambalo pia ni mwanachama wa mataifa yenye kuzalisha kwa wingi mafuta OPEC, linalokabiliwa na kuporomoka kwa bei ya mafuta na kadhia ya janga virusi vya corona.

Post a Comment

0 Comments