TANGAZA NASI

header ads

Uhamiaji watoa onyo kali wanaoingiza wahamiaji haramu hapa nchini

 


Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji hapa nchini Dkt Annah Makakala amewaonya wananchi wanaojihusisha na biashara haramu ya usafirishaji wa wabinadamu, wahamiaji haramu kuacha mara moja kwani vitendo hivyo ni hatari kwa usalama wanchi na raia wake.


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Kamishna jenerali wa Uhamiaji Dkt Annah Makakala amesema kitendo cha kuingiza raia wa kigeni hapa nchini kinyemela ni jambo la hatari sana kwa usalama wanchi.


“Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wahamiaji haramu wanaoingia nchini kwa makundi kupitia njia zisizo rasmi wakitoka katika pembe ya Afrika, tumepata taarifa kuwa wahamiaji hao wanasaidiwa na baadhi ya wananchi wasiokuwa wazalendo kwa nchi yao” amesema Dkt Annah Makakala.


Amesema kitendo cha wananchi hao kuendelea na biashara hiyo haramu ni hatari kwa sababu wahamiaji wengi wanapoingia huanza matukio ya kihalifu na kutumia siraha pia wanaikoseshea mapato serikali yao, huku akitaja nchi za Ethiopia, Eritria na Somalia ndizo zinazoongoza.


Amesema jeshi la uhamiaji kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama wataendelea  kufuatilia baadhi ya wananchi ambao wanajihusisha na vitendo hivyo na pindi wakibainika kufanya uhalifu huo watachukuliwa hatua za kisheria ambapo adhabu yake ni kifungo miaka 20 au faini ya shilingi million 20 au vyote kwa pamoja.


Ameongeza kuwa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tangu mwezi Januari hadi Novemba, 2020  wamefanikiwa kuwa kamata raia 45 wa Tanzania wanaojihusisha na vitendo hivyo pamoja na kushikilia magari 13, Boti 2 na pikipiki 16 zinazojihusisha na biashara hiyo.


Aidha amesema kwa kipindi hicho wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 15, 266 ambao waliingia hapa nchini bila kufuata taratibu za kiuhamiaji na tayari wamechukuliwa hatua mbalimbali za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani.


Katika kukabiliana na tatizo la uhamiaji harama wanatarajia kuanza kutoa elimu katika shule ngazi zote ili kukomesha tatizo hilo watoto wanapokua wajue madhara ya kuingiza wahamiaji haramu ni kosa pia ni hatari kwa usalama wa nchi.

Post a Comment

0 Comments