Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ametoa muda wa saa 72 kwa vikosi vya mkoa wa Tigray kujisalimisha kabla ya jeshi la shirikisho kuanza kuushambulia vikali mji mkuu wa Mekelle.
Waziri mkuu Abiy ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter akiwataka wapiganaji wa Tigray kujisalimisha kwa amani, wakitambua kuwa hakuna kurudi nyuma.
Mapema jana Jumapili, jeshi la Ethiopia lilitishia kuuzingira mji wa Mekelle unaokaliwa na maelfu ya raia. Msemaji wa jeshi la Ethiopia Dejene Tsegave amewaeleza wakaazi wa mji huo kujiokoa na kujiweka mbali na wanajeshi wa mkoa.
Hata hivyo kiongozi wa chama tawala cha Tigray TPLF, Debretsion Gebremichae ameahidi mapiganao makali kulizuia jeshi la shirikisho kusonga mbele.
0 Comments