TANGAZA NASI

header ads

Mwanahabari avamia mkutano wa siri wa baraza la EU

 


Mwanahabari wa Uholanzi amehudhuria mkutano wa siri wa Baraza la Mawaziri wa Ulinzi Mataifa ya Jumuiya ya Ulaya (EU) kupitia mtandaoni bila idhini.

Kwa mujibu taarifa za shirika la RTL Nieuws, mwanahabari Daniel Verlaan alitumia nywila ya tarakimu 6 ambapo aligundua tarakimu 5 za mwanzo kupitia picha iliyochapishwa mtandaoni na Waziri wa Ulinzi wa Uholanzi Ank Bijleveld.

Baada ya majaribio ya mara kadhaa na kufanikiwa kujiunga na mkutano huo, Verlaan, aliwapungia mkono kwa kucheka mawaziri. Wakati huo huo, kituo cha habari cha RTL Nieuws pia kiliweza kumuona mwanahabari huyo.

Baada ya kumuona Verlaan, Mwakilishi wa EU wa masuala ya nje na sera za kiusalama Josep Borrell ambaye alikuwa akiongoza mkutano huo alimuuliza, "Unajuwa kuwa umeingia mkutano wa siri bila idhini?"

Mwanahabari wa Uholanzi naye akajibu, "Ndio, naomba samahani. Mimi mwanahabari wa Uholanzi. Mniwie radhi kwa kuingilia mkutano wenu. Naondoka sasa."

Borrell alimwambia tena kwa kucheka, "Unafahamu kuwa hili ni kosa ama sivyo? Itakuwa vyema kujiondoa kabla polisi hawajafika."

Afisa mmoja wa EU aliarifu kuwa mkutano ulimalizika. Pia aliongezea kusema kuwa kitendo cha kuingilia mkutano bila idhini ni kinyume cha sheria na ataripoti kwa mamlaka husika.

Post a Comment

0 Comments