Oktoba 25,2020 Zikiwa zimesalia siku Tatu Kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Kumchagua Rais , Wabunge na Madiwani Nchini Tanzania Oktoba 28,2020 , Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Wakili Joseph Kamonga ameendelea na Mikutano ya Kampeni za Kumuombea Kura Rais Dkt John Pombe Magufuli na Madiwani wa CCM.
Akiwa Kata ya Lupanga Kijiji cha Utilili Wilayani Ludewa Mhe.Kamonga amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Rais Dkt John Pombe Magufuli kwani amefanya kazi nzuri na Ludewa anaijali ametupa Fedha nyingi kuliko Wilaya yeyote ya Mkoa wa Njombe.
''Ndugu zangu nasimama mbele yenu kwa heshma kubwa kumuombea Kura Rais Dkt John Pombe Magufuli kwasababu ni kipenzi cha watu na Ludewa anaijali , anatujengea Rami ya Kiwango cha Kimataifa ameanza na Kilimeta hamsini lakini lengo lake ni kumaliza kutoka Itoni hadi Manda katika Mkoa huu Wilaya Iliyopata Fedha Nyingi za Magufuli ni Ludewa , kwenye Barabara hii ametoa zaidi ya Bilioni 167 ''.amesema Mhe.Kamonga
Mbunge huyo ameongeza Kusema Kuwa ''Kwenye sekta ya Afya Wilaya ya Ludewa Rais Magufuli ametuletea Bilioni 3.3 nyingi zimekwenda kwenye Vituo vya afya na Zahanati , Sekta ya Umeme ametupa bilioni 9 ambapo kwenye Rea bilioni 5 zimeingiza umeme Ludewa katika Vijiji 77 vimesalia vijiji 14 pekee kupata Umeme na Bilioni 3 Umeme Wa Gridi Ya Taifa, Kwenye Sekta ya Elimu ameleta bilioni 29 kugaramia Elimu bila malipo matokeo yake kiwango cha ufaulu Ludewa Kimepanda Kutoka asilimia 63 wakati anaingia hadi kufikia asilimia 85 kuna changamoto ya Walimu na tayari Rais Magufuli ametangaza Ajira za Walimu 13000 , nimechunguza Ludewa Tunaupungufu wa Walimu 421 Shule ya Msingi na 71 Sekondari na ameahidi kwamba miaka hii mitano anakwenda kushughurikia swala la Ajira Kwa Vijana''.
Katika hatua nyingine Wakili Kamonga akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Itundu Kata ya Mlangali amewaahidi Kuupanga vizuri mji huo na kuurasimisha kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoishi katika eneo hilo , huku akiwahakikishia kutatua changamoto ya mgao wa umeme unaowakumba wananchi hao.''Zamani tulikuwa tunasema Mlangali ni Pazuri kuliko pale Wilayani Ludewa na watu wa hapa ni Wachapakazi , Mlangali ingewahi kupata umeme ingekuwa mbali sana , Ndugu zangu hili la Mgao wa Umeme linanikera linanikwaza sana'' amesema Mhe.Kamonga.


0 Comments